Ezra 7:21-24

21 aMimi, Mfalme Artashasta, sasa naagiza watunza hazina wote wa Ngʼambo ya Mto Frati kutoa kwa bidii chochote kwa Ezra kuhani na mwalimu wa Sheria ya Mungu wa mbinguni atakachohitaji kwenu, 22talanta 100
Talanta 100 za fedha ni sawa na kilo 3,400.
za fedha, ngano kori 100,
Kori 100 za ngano ni sawa na kilo 10,000.
divai bathi 100,
Bathi 100 za divai ni sawa na lita 2,000.
mafuta ya zeituni bathi 100, na chumvi kiasi chochote.
23 eChochote ambacho Mungu wa mbinguni ameagiza, kifanyike kwa ukamilifu kwa ajili ya Hekalu la Mungu wa mbinguni. Kwa nini pawepo ghadhabu dhidi ya utawala wa mfalme na wanawe? 24 fPia ninyi fahamuni kuwa hamna mamlaka ya kuwatoza kodi, ushuru au ada makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, watumishi wa Hekalu au wafanyakazi wengine kwenye nyumba ya Mungu.

Copyright information for SwhNEN